Makala ya Kiswahili
Kiswahili ni lugha ya taifa na pia lugha rasmi. Kama lugha ya taifa, inawa ung anisha wa t u wa makabila tofauti na kuwashirikisha katika shughuli za kujenga nchi. Kama lugha rasmi, inatumika katika shughuli zote za serikali kama vile bungeni, mahakani na kadhalika.
Hapa katika shule ya upili ya Kabare Girls', Kiswahili ni moj awapo y a somo linaloenziwa na kuonewa fahari na wanafunzi. Wanafunzi wengi hutia fora katika somo hili na hivyo basi huchangia pakubwa katika kuinua na kuboresha hali ya Kiswahili kama somo.
Wanafunzi wengi hujitolea kuwakilisha shule yetu katika warsha mbalimbali nchini zinazoandaliwa ili kuboresha somo hili na huibuka miongoni mwa wanafunzi bora.
Hapa shuleni mna idara ya Kiswahili inayoongozwa na Bi. Elizabeth Wanjiru Njeru kama mkuu wa idara. Pia mna timu ya walimu waliobobea katika lugha hii. Wanafanya kazi kwa ushirikiano na wana mlahaka mwema miongoni mwao na hivyo huigwa na wanafunzi ambao hutia bidii za mchwa katika utendakazi wao.
Walimu hawa wana tajriba ya hali ya juu na wana umilisi wa kutosha katika kushughulikia masuala mbalimbali katika somo la Kiswahili. Wanaidaira hufanya kazi yao kwa dhati ili kuhakikisha kuwa masilahi ya wanafunzi yamepewa kipaumbele.
Lugha ya Kiswahili huwa miongoni mwa masomo yanayopata matokeo bora Zaidi hapa shuleni. Mwaka uliopita KCSE tulizoa alama ya 10.223 B+. Wanafunzi wengi pia huendelea na somo la Kiswahili hadi chuo kikuu na mwishowe huja kujiunga na kazi ya ualimu bila kuwaogopa walimu wao hivyo basi hutoa mchango wao wa kuinua Kiswahili juu zaidi.